Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Hakuna msanii aliyeshtaki mahakamani kudhulumiwa na Wasafi

Baba Levo 24324 Baba Levo: Hakuna msanii aliyeshtaki mahakamani kudhulumiwa na Wasafi

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni Chawa wa Diamond Platnumz, Baba Levo amesema hakuna msanii wa Lebo ya WCB ambaye amewahi kwenda mahakamani kudai kuwa amedhulumiwa kwani lebo hiyo inafuata misingi ya sheria na makubaliano wanayojiwekea na msanii husika.

Baba Levo amesema hayio kufuatia kauli ya producer P Funk kuwa WCB inawagandamiza wasanii wake na kuwadhulumu mpaka kusababisha kujiondoa.

"Hakuna msanii aliyedhulumiwa WCB, ukifanya kazi kwa mkataba inakuonyesha kabisa ukidhulumiwa unaweza kwenda kwenye vyombo vya sheria ukaomba haki yako.

“WCB wanapokusainisha mkataba wanajua kuna siku utahitaji kuondoka ndio maana wameweka kipengele maalum kinachosema ukitaka kuondoka unatakiwa kufanya hivi na hivi, wangekuwa hawataki msanii aondoke wangesema hakuna msanii kuondoka," amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live