Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Akifa Diamond nitalia kuliko Zuchu

Baba Levo Mondi Zuchu Baba Levo: Akifa Diamond nitalia kuliko Zuchu

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba Levo au Fundi Manyumba kama anavyopenda kujiita; ni komediani, msanii wa Bongo Fleva na mtangazaji ambaye huwa haishiwi amshaamsha ambaye safari hii amezua mapya kabisa kuhusu uwezekano wa Diamond Platnumz kuwa katika uhusiano na msanii wake, Zuchu.

Baba Levo anasema kwamba Diamond akifa atabubujikwa zaidi na machozi kuliko Zuchu ambaye kwa siku za hivi karibuni ameonekana kuwa na ukaribu usio wa kawaida na Diamond.

Baba Levo hajaweka wazi kama anamtakia Diamond kifo au vipi, lakini amefafanua kwa kiduchu tu kwamba kulia kwake kwa wingi mpaka atwae Tuzo ya Mwombolezaji Bora zaidi ya mtu yeyote yule ni kwa sababu ya heshima yake kwa Diamond ambaye amemsaidia na kumuamini wakati hakuna mtu alitaka kufanya kazi na yeye.

“Daimondi akifa nitalia kuliko Zuchu..!! Maana tangu ameanza kunisaidia maisha yangu na watoto wangu yamebadilika kabisa. Thanks @diamondplatnumz

Chanzo: www.tanzaniaweb.live