Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Davido atia neno mwanae kukosa Grammy

Davido Reveals What Happened When His Father First Saw Tattoos Baba Davido atia neno mwanae kukosa Grammy

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kushindwa kunyakuwa tuzo yoyote katika vipendele vitatu alivyoteuliwa na Grammy mkali wa Afrobeat Davido ameeleza kuwa licha ya kukosa Tuzo hizo baba yake mzazi Adedeji Adeleke anaamini kuwa mwanaye ni mkali.

Kufuatiwa na maohijano yake aliyoyafanya na ‘Rolling Stone’ ameeleza kuwa kuteuliwa pekee kulitosha kabisa kumfanya ajivunie, huku akidai kuwa baada ya kutoka katika Tuzo hizo baba yake alimpigia simu na kumwambia kuwa haijalishi nini kilitokea lakini anaamini mwanaye bado ni ‘Legend’.

Siyo Davido pekee ambaye hakuondoka na Tuzo hizo, wapo mastaa wengine kutoka Nigeria akiwemo Burna Boy, Asake, Ayra na wengineo.

Tuzo za Grammy zilitolewa siku ya Jumapili Februari 4 katika ukumbi wa ‘Crypto.com Arena’ Los Angeles nchini Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live