Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya kuzinguana na Drake kwenye video ya ‘Come Closer’, Wizkid achukua maamuzi mazito

5065 Wizkid 5 1 TZW

Tue, 20 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Kwa mashabiki wa muziki hususani muziki wa Nigeria watakumbuka kuwa kwenye video ya ‘Come Closer’ ya  Wizkid aliyomshirikisha Drake kutoka Marekani, Msanii huyo hakuonekana kwenye kichupa hicho kitu ambacho kiliibua maswali mengi na baadhi ya mashabiki kumshambulia Wizkid.

Tokeo la picha la wizkid

Wizkid

Sasa ukweli ni kwamba ingawaje walizinguana na baadaye kuonekana kupatana ukweli ni kwamba kitendo cha Drake kutoonekana kwenye video hiyo bado kilikuwa kinamuumiza sana Wizkid mpaka leo.

Wizkid amesema kuanzia mwaka huu hata’shoot tena video yoyote ile nje ya bara la Afrika na video zote ambazo amesha’shoot nchini Marekani hataziachia.

Akizungumza kwenye mahojiano yake Jumamosi iliyopita na kituo cha Redio cha The Beat 99.9 FM cha nchini Nigeria, Wizkid amesema maamuzi hayo aliyapanga toka mwaka jana baada ya kuona hakuna umuhimu wa kupoteza hela nyingi kwa ajili ya ku’shoot video ughaibuni.

Nimeamua kwa sasa sita’shoot tena video zangu nje ya nchi, Nataka nifanyie video zangu na kila kitu hapa hapa Afrika, Kwa hiyo hata video zangu nilizo’shoot mjini Los Angeles (Marekani) sitazitumia tena,“amesema Wizkid baada ya kuulizwa swali lililohoji kwanini kwenye albamu yake ya ‘Sound From The Other Side’ hakuna hata video moja.

Hata hivyo, taarifa hizo hazijapokelewa vizuri na mashabiki wake huku wengi wakihusisha maamuzi hayo kuwa yamekuja baada Drake mwaka jana kutoonekana kwenye video ya Come Closer.

Chanzo: bongo5.com