Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya afya kukaa sawa! Profesa Jay ateta na Joseph Kusaga

Kusaga Jayyy06 Joseph Kusaga na Joseph Haule.

Sun, 17 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Hip Hop nchini Tanzania, Joseph Haule maarufu kams Professor Jay amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Clouds Media Group (CMG) na mdau mkubwa wa masuala ya burudani nchini, Joseph Kusaga ikiwa ni baada ya afya ya staa huyo kuimarika.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Professor Jay ameandika; "Ilikua furaha sana kwa siku ya jana, kutenga sehemu ya muda wangu, kufanya mazungumzo na mdau mkubwa wa sanaa nchini kwetu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Kaka yangu na rafiki yangu wa siku nyingi, Joseph Kusaga na kumpa shukrani zangu kwa support yake kubwa sana aliyoitoa kupitia vyombo vyake vya habari kwa kipindi chote nilichokuwa kwenye matibabu.

"Lakini pia tumejadiliana masuala mbalimbali kuhusu Taasisi ya Professor Jay Foundation na namna tutakavyoshirikiana kuwezesha masuala mbalimbali yenye manufaa kwa jamii," amesema Profesa Jay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live