Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Rayvanny kusepa, WCB yatangaza kusaini wasanii wapya wawili

Babu Tale Na Diamond.png WCB yatangaza kusaini wasanii wapya wawili

Tue, 16 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lebo ya WASAFI inayomilikiwa na msanii maarufu Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ imetangaza kuwa hivi karibuni itasaini wasanii wengine wapya wawili ikiwa ni miezi michache baada ya msanii wao, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ kuondoka ndani ya Lebo hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meneja wa WCB, Hamisi Taletale ‘babu Tale’ amesaini utiaji saini wa mikataba hiyo utashuhudiwa na BASATA na COSOTA kwani ndiyo vyombo maalum vya Serikali vinavyosimamia tasnia ya Sanaa nchini.

“Hivi karibuni tuta sain wasanii wawili kujiunga lebo ya WASAFI ila safari hii tumeamua msanii atakua na mashaidi wawili kutoka COSOTA na BASATA. Music ni biashara yetu na nijukumuletu kukuza na kusimamia hii kazi atuwezi kuacha hata iwe vipi. #theblackgodfather,” amesema babu Tale.

Ikumbukwe kuwa, mwezi Aprili mwaka huu, 2022, wakati akihojiwa na Shirika la Utangazaji la BBC kupitia kwa mtangazaji wake, Salim Kikeke, CEO wa WCB, Diamond alisema mwaka huu watasaini wasanii wawili na wengine wataondoka.

“Mwaka huu tunakwenda kutambulisha wasanii wawili, na sio kila msanii aliyepo WCB ataendelea kuwepo, wengine wataondoka waanze kujitegemea. Lazima tuwaunge mkono na kuwasapoti, tusiwatengenezee kama ni vita ama chuki na Diamond.

Utakumbuka WCB Wasafi haijasaini msanii mpya tangu Aprili 2020 walipomtangaza Zuchu ambaye alikuwa msanii wa pili wa Kike ndani ya lebo hiyo.

Tayari mpaka sasa, Rayvanny, Harmonize na Rich mavoko wameshaondoka ndani ya Lebo hiyo maarufu Barani Afrika. Mbali na Diamond wasanii waliopo WCB kwa sasa ni Zuchu, Mbosso, Lavalava na Queen Darleen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live