Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Kuombwa Talaka, Kiba Asema "Nakupenda sana Usinisahau"

Alikiba Wife Amina Khalif Baada ya Kuombwa Talaka na Mkewe, Kiba Asema

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

IKIWA ni saa kadhaa baada ya kusambaa kwa taarifa kutoka nchini Kenya zikidai kuwa mke wa supastaa wa Bongo Fleva, Alalikiba aitwaye Amina ametaka talaka akidai kuwa mumewe huyo hatimizi majukumu yake kama mume/ baba katika familia, Kiba ameibuka na hili jipya.

kupitia ukurasa wake wa Instagram, ikiwa leo kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa mtoto wake, Keyaan, Kiba amempost na kuandika; "Halizuki jambo bila Mwenyezi Mungu kutaka yote kheri, happy birthday son nakupenda sana usinisahau @keyaanalikiba #kingkiba''

Imeelezwa kuwa, mke wa Kiba amekwenda katika mahakama ya kadhi akitaka apewe talaka na muewe huku pia akiiomba mahakama hiyo iamwamuru Kiba kutoa Tsh milioni 4 kila mwezi kwa ajili ya matumizi ya watoto wake wawili aliozaa na mwanamke huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live