Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Kajala, Harmonize sasa amgeukia House Girl wake

Harmonize 56 Zuwena Harmonize na Zuwena

Sun, 8 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ameahidi kumzawadia mjakazi wa ndani Zuwena nyumba na gari.

Amepiga hatua hiyo kama ishara ya shukrani kwa huduma alizomtolea katika kipindi cha miaka saba ambacho kimepita. Konde Boy ametangaza kuwa anapanga kutimiza hadi yake kwa Zuwena kabla ya mwezi wa Mei kuisha.

"Ni kama shangazi yangu. Miaka 7 anajua nakula nini. Ananipikia, ananifulia, ananifanyia usafi, anajua ukichaa wangu wote. Kabla ya Juni namnunulia gari lake la kwanza na kinyumba hata cha chumba 3 mkoani kwao," Harmonize alitangaza kupitia Instagram.

Harmonize amefichua kuwa Zuwena ndiye mjakazi wake wa kwanza huku akidai kuwa sio kijakazi wake tu bali pia ni kama dada yake huku akimshukuru mwanadada huyo kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akifanya na kumtakia baraka za Maulana.

"Mungu akubariki dada Zuuh maana si kwa vipipi vya sigara ambavyo unavifagia kila siku kwenye mashuka majivu vipi," aliandika mwanamuziki huyo na kuambatanisha ujumbe wake kwa video ya Zuwena akiwa jikoni akipakua chakula.

Siku za hivi majuzi Harmonize amekuwa akiwanunulia watu wa karibu naye magari kwa sababu tofauti. Tayari amemnunulia magari mawili aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja akiwa na nia ya kuomba msamaha na kurejesha mahusiano ya.

Mapema wiki hii alimnunulia mama yake mzazi gari aina ya Harrier na kufichua kuwa hiyo ndiyo gari aipendayo zaidi. Mwezi uliopita alimnunulia gari ndogo mpiga picha wake Jabulant.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live