Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Baada Nigeria kupigwa marufuku Dubai, Tanzania yapewa nafasi

Sf Mwezi D Baada Nigeria kupigwa marufuku Dubai, Tanzania yapewa nafasi

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kutangaza kufungia visa raia wa Nigeria mnamo Oktoba 2022, Bodi ya utalii ya Dubai imehamishia nguvu yao kwa nchi nyengine za Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Afrika Kusini.

Dubai imetambulisha mabalozi wanaowakilisja nchi hizo akiwemo msanii wa Afrika Kusini, Thabsie na msanii kutoka Kenya Bahati.

Hata hivyo bodi ya utalii Dubai inaendelea kutafuta mabalozi wengine wa kuwakilisha nchi hizo katika kutalii Dubai.

Mabalozi hao wanategemewa kutumia umaarufu wao kuonesha watu wa nchi zao vitu ambavyo vinapatikana Dubai ili kuwavutia na wamejiunga na kampeni inayoitwa A to Z of Dubai inayoonesha watalii vitu vizuri vya Dubai.

Ripoti zinaeleza pia kwamba aliekua Rais wa Nigeria, Muhammad Buhari ameomba Dubai waondoe zuio la visa Wanigeria na kuonesha utayari wa kuzungumza juu ya tofauti zao na kuweza kuwakaribishia Wanigeria nchini humo tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live