Nairobi, Kenya. MPENZI wa Diamond Platinumz msupa Mkenya, Tanasha Donna kajitetea baada ya kutolewa rangi kinoma na wengi alichemsha kinoma kwenye pati ya uzinduzi wa EP DonnaTella.
Mastaa kibao wa muziki hapa nchini walihudhuria hafla hiyo katika Ukumbi wa Sarit Center Expo kwa ajili ya kumpa sapoti Jumamosi iliyopita. Hata hivyo, ukweli wa mambo ni uzinduzi wa EP hiyo haukuvutia kabisa wengi wakimtoa rangi Tanasha kwa kushindwa kujipanga.
Utumbuizaji wake ulikuwa wa kama vile mtu anayejifunza kuimba. Mara kwa mara aliimba nyimbo zake nje ya biti. Hakukuwa na mvuto wala msisimko jambo ambalo lilipelekea wengi kumtoa rangi.
Wengine walidai kuwa ili kuepuka fedheha, ndio sababu mpenzi wake Diamond Platinumz aliamua kurudi nyumbani kwao kwenye siku ya uzinduzi kwa kile walichodai kisingizio cha jambo la dharura la kifamilia.
Hata hivyo, akijibu mapigo, Tanasha kadai hakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa na kuahidi kujipanga vizuri zaidi wakati mwingine.
“Kwa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanya kitu kama kile, naaamini nilijitahidi ukizingatia nilikuwa na siku mbili tu ya kufanya mazoezi. Ila najua nilipaswa kujitahidi hata zaidi” Tanasha kajitetea.
Pia Soma
- BURUDANI: Wema Sepetu afunguka alivyotoa mimba mbili za Kanumba, akata tamaa kupata mtoto
- Chid Benz amjia juu Harmonize
- BURUDANI: Nick Minaji na mchumba wake kugawa kichapo