Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BASATA yafafanua sakata la Diamond kujitoa Tuzo za TMA

Diamond Eppp Diamond Platnumz

Sun, 20 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara baada Baraza la Sanaa Tanzania kutoa orodha ya wasanii watakaowania Tuzo za Muziki Tanzania "Tanzania Music Awards" 2021, mijadala mbalimbali imejitokeza mitandaoni kwanini hakuna wasanii wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) kwenye orodha hiyo.

Kaimu Katibu Mtendaji BASATA, Matiko Mniko amesafisha wingu na kusema kazi zilizowekwa kwenye kinyang'anyiro hicho ni zile zilizokusanywa na wasanii wenyewe.

"Kazi hizi zilizochujwa na kuja na 'nominee' ni zile zilizowasilishwa na wasanii wenyewe. BASATA (Serikali) tuliamua kuweka wazi kila mmoja aamue yeye mwenyewe kushiriki. Kwahiyo kuna wengine kwa sababu moja au nyingine wanaweza wasiamue kushiriki, lakini waliojitokeza kushiriki ni wengi zaidi," amesema Mniko

Aidha, Mniko amesema wamepokea kazi takribani 1360 zilikusanywa kuwania tuzo hizo.

Katika kinyang'anyiro cha Msanii Bora wa Kiume yupo Jux, Marioo, Whozu, Harmonize na Ben Pol.

Best Female Bongo Fleva Artist (Msanii Bora wa Kike Bongo fleva) wapo Sarafina, Rosa ree, Anjella na Marry G. huku nafasi ya Mwanamuziki Bora wa kike wa mwaka ikiwaniwa na Christina Shusho, Frida Amani, Nandy na Joyce Mwaikofu.

Kwa upande wa wasanii Bora Chipukizi wa kiume wakichuana uso kwa uso ni Kusah, Kinata MC, Lody Music, Rapcha na Damian Sol.

Profesa J ni miongoni mwa wasanii walioorodheshwa kwenye mkeka huo akiwania Tuzo ya msanii bora wa Hiphop, huku wimbo wake wa 'Utaniambia Nini' ukiwania kuwa wimbo bora wa hiphop wa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live