Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BASATA wamuachia Dudubaya

46a5ea9cdc72fec0dd9ce95eefebc01d BASATA wamuachia Dudubaya

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BARAZA la Sanaa la Taifa Tanzania (Basata) imemfungulia msanii wa Bongo fleva , Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ baada ya kuomba radhi kwa kosa la kutumia lugha ya matusi mtandaoni.

Dudubaya alifungiwa na Basata, Aprili 17, 2020 hii ikiwa mara ya pili kwa msanii huyo kukutana na rungu la wasimamizi hao wa sanaa.

Awali, mapema Januari 7, Dudubaya alifutiwa usajili na baraza hilo baada ya kugoma alipoitwa kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili lakini Februari mwaka jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wakati huo Dk Harrison Mwakyembe alitangaza kumsamehe huku akiahidi kujirekebisha.

Katika barua iliyotolewa juzi na kaimu katibu wa baraza hilo Matiko Mniko ilisema kuwa imemfungulia msanii huyo na yuko huru kushirikiana na wasanii wengine lakini kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.

“Baraza linawakumbusha wasanii na wadau wa sanaa nchini kufanya kazi kwa weledi kuzingatia maadili na kuongeza ubunifu ili kuongeza tija kwenye tasnia,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz