Siku chache zilizopita stori kubwa katika Mitandao ya kijamii na Ulimwengu wa Burudani Tanzania ilikuwa Malalamiko ya Staa wa Muziki Harmonize akidai kuwa Lebo yake ya zamani ya WCB na kampuni ya Ziiki wameshirikiana kutaka kuharibu maisha yake.
Mbali na hivyo alidai kuwa hajawahi kupokea Pesa ya aina yoyote kwenye kazi zake Miaka 7 sasa na Lebo yake ya zamani imekuwa ikizikusanya pesa hioz licha ya kuwalipa Milioni 600 kumalizana nao.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema kuwa halijapokea malalamiko yoyote kutoka kwa Staa huyo hivyo haliwezi kusemea chochote kwani Msanii anatakiwa afikishe malalamiko ofisini ndio yafanyiwe kazi.
Katibu Mtendaji wa Basata DKT. Kedmon Mapana Amesema kuwa msanii yeyote anayehitaji msaada kwa Baraza atachukuliwa kwa uzito na kusaidiwa.