Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BASATA kushika mkono Madam Ritha

WhatsApp Image 2022 10 20 At 6.jpeg BASATA kushika mkono Madam Ritha

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: VOA

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeahidi kumshika mkono Muandaaji wa Shindano la kusaka vipaji vya kuimba Bongo star search (BSS) Ritha Paulsen maarufu Madame Ritha ili kutimiza ndoto za vijana hao pindi shindano linapoisha.

Akizungumza jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt.Kedmon Mapana wakati wa uzinduzi wa Shindano la (BSS) Msimu wa 13 ambao umebeba kauli mbiu 'Nyota kama zote' amesema anatambua mchango mkubwa unaofanywa na Kampuni ya Benchmark kwa zaidi ya miaka 13 katika kusaidia vijana wengi kuonyesha vipaji vyao.

Mapana amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imemchagua kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika sekta ya sanaa ili vipaji viwe vinapewa thamani na wanaahidi Shindano hilo kulishika mkono ili vipaji vingi vizaliwe

Hata hivyo Mapana ameweka wazi kuwa watamshika mkono jaji mkuu na Muandaaji wa Shindano hilo kwa kuhakikisha Mshindi wa kwanza anapatiwa pesa taslim shilingi milioni 5 kama zawadi.

Kwa upande wake Muaandaaji wa Shindano la BSS Ritha Paulsen amesema kupitia Shindano la BSS limekua likigusa zaidi ya Vijana 5000 na kuwaokoa kutokana na uwepo wa Kampeni ya kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi huku zaidi ya watanzania milioni 60 wanafatilia show hiyo kupitia st swahili kwenye King'amuzi cha Startimes.

"Naweka wazi na kunadi kuwa Bongo star search (BSS) ndio kipindi pendwa kinachotazamwa na watu milioni 60 kutokana na maudhui mbalimbali yanayooneshwa kuanzia kambini washiriki wanavyoishi,wakufunzi wanavyowafunza namna ya kutumia sauti zao pamoja na mchakato mzima wa kupatikana kwa washiriki hao mikoani."

Paulsen ameeleza kuwa Msimu wa 13 utakua wa kitofauti zaidi ili kuboresha Shindano hilo liwe na mvuto zaidi."Misimu yote imekua ikiboreshwa hivyo msimu wa 13 kuna ingizo jipya la majaji ambao wasanii wakubwa kutoka kiwanda cha Muziki wa Bongofleva akiwemo Rayvan, Nandy,Shilole,Fid q,Barnaba pamoja na Jux."

Pia amempomgeza Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt.Mapana kwa kusikia changamoto wanazokutana nazo na kuomba kushikamana na kufanya kazi kwa pamoja ili Vijaya waweze kufikia malengo yao na kuzalishwa kwa wasanii wengi wenye uwezo wa vipaji vyao kuonekana zaidi.

"Hatuhitaji fedha tunahitaji Ushirikiano kutoka Serikalini kwani BSS ni sehemu ambayo vipaji vinaibuka lakini Kampuni haina uwezo wa kuendeleza vipaji vyao wakiwa kama walezi wetu na wadau wakubwa. "

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Startimes limited David Malisa amesema waliweza kuchukua nafasi ya kipekee takribani miaka 4 ambapo imekua ya kitofauti na kutazamwa na watanzania wengi kutokana na ubora wa maudhui yanayoletwa kwa mtazamaji.

Malisa ameongeza kuwa Shindano hilo litaanza kuruka Oktoba 30 mwaka huu chaneli ya St Swahili kupitia kifurushi cha chini cha nyota au kupitia programu ya simu ya mkono "Startimes on" Ametoa mwito kuwa wataendelea kuwajali wateja wao kuendelea kuwasogezea maudhui mara 100 zaidi kwa bei rafiki kwenye ving'amuzi vyao.

Chanzo: VOA