Mtangazaji wa kituo cha Efm, B-Dozen awajibu wanaodai pengine amehusika katika kuteua Nominees wa Tuzo za Muziki Tanzania (Tanzania Music Awards), amefunguka kupitia instastory baada ya watu wengi kumuona akisherehesha shughuli ya kuwatambua Nominees wa TMA mwaka 2022 na wengi wakiamini kuwa ni moja wa wajumbe waliohusika kuteua Wasanii.
“Let Me Make It Clear. Sihusiki kwa namna yoyote na wateule wa Tuzo #TMA Mimi kazi yangu ilikua ni ku host tu, (kuongoza shughuli) Majina na Wateule nimeyaona kama wewe ulivyoyaona. Ahsante!” Aliandika B Dozen
Tuzo hizo zimeonekana kukosolewa na wasanii wengi baada ya kutangazwa kwa vipengele vinavyogombaniwa.