Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki na Mobeto watinga ukumbini kimahaba

Aziz Ki Na Mobeto Watinga Ukumbini Kimahaba.png Aziz Ki na Mobeto watinga ukumbini kimahaba

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa kuamkia leo Agosti 2, 2024, ilifanyika halfa ya utoaji tuzo mbambali kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika msimu wa 2023-24 ambapo wachezaji sambamba wadau mbalimbali wa michezo, waliweza kutunukiwa.

Ukiachana na hilo, miongoni mwa matukio ambayo yaligusa hisia za wadau wengi hususan wa burudani na michezo, ni kitendo cha mrembo Hamisa Mobeto kuingia katika ukumbi wa Super Dome akiwa beneti na kiungo huyo mshambuliaji wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki.

Hamisa ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa akionekana kwenye viwanja mbalimbali vya burudan na Aziz Ki, mara kadhaa amekanusha kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na nyota huyo wa Kimataifa kutoka Burkinafaso.

Vilevile, Aziz Ki naye amehojiwa hivi karibuni na kudai Mobeto ni rafiki yake tu hakuna kinachoendelea licha ya kuwa ukaribu wao umeendelea kuibua maswali mengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live