Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ayra Starr ameajiri familia yake yote

Ayra Starr Db7107 Oyinkansola Sarah Aderibigbe, maarufu kama Ayra Starr.

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii kutoka nchini Nigeria, Oyinkansola Sarah Aderibigbe, maarufu kama Ayra Starr, ameajiri karibu kila mtu kwenye familia yake baada ya kupata umaarufu, Ndugu zake wote wanafanya kazi naye na wanalipwa moja kwa moja na lebo ya Mavin Records.

Kaka yake (Bushboy Marc) ni muongozaji wa video na anawajibika kwa video zake nyingi za muziki, Anapata asilimia ya mapato ya video za muziki ambayo ina maana kwamba anapata mamilioni kutokana na kuziongiza nyimbo zake maarufu kama vile "Bad Vibes" na nyinginezo.

Dada yake (Saltiana) ni DJ na anafanya kazi kama DJ binafsi wa Ayra Starr, Anaongozana naye kwenye maonesho yake na matamasha yake yote na kumtangaza kote Ulimwenguni.

Ndugu yao mdogo (Milar) ni msanii na mtayarishaji wa Muziki/ mwandishi, Anamsaidia Ayra Starr kuandika na kutengeneza nyimbo zake na kulipwa kwenye kila kazi yake na pia dada yake mkubwa anajifunza biashara ya muziki kupitia Mavin Academy.

Mama yao ndiye mshauri wa kila kitu kwenye Muziki wa Ayra Starr na humpa ruhusa kabla hajafanya maamuzi yoyote, ikiwa ni pamoja na kusaini mikataba, mikataba ya kupata ubalozi wa chapa mbalimbali, na kusimamia mirabaha yake.

Familia yake ndiyo humfanya Ayra Starr kuwa na nguvu, Ndugu zake wanamtia moyo na wako kila wakati kumsaidia kila wakati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live