Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Awilo afichua kilichomleta

49b36434b8b90a12c9e6631f6951ca23.jpeg Awilo afichua kilichomleta

Wed, 12 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI wa dansi Awilo Longomba amesema sababu iliyomfanya kuja Tanzania ni kujitangaza kupitia sanaa yake.

Akizungumza katika mahojiano maalumu, Dar es Salaam jana, Longoma alisema amekuja Tanzania mara mbili, mara ya kwanza ilikuwa kwa ajili ya kutengeneza filamu ambayo alikuwa mwigizaji mkuu.

“Mara ya kwanza kufika Tanzania nilikuja kupiga picha za filamu ambayo awali ilikuwa ifanyike London na binafsi nikaichagua Tanzania maana nilikuwa kama muigizaji mkuu,” alisema Awilo.

Alisema alitaka filamu yake apige picha akiwa Mlima Kilimanjaro au mbuga za wanyama Serengeti lakini ilishindikana kwa sababu ya muda kuwa mfupi.

Alisema mara ya kwanza kusikia muziki wa Tanzania ilikuwa Kinshasa na ulikuwa wimbo maarufu kutoka Tabora Jazz mwaka 1974 unaoutwa Dada Asha.

Naye msanii Angelmary Kato ambaye ndio mwenyeji wa Awilo kwa sasa alisema anaona kama ni ndoto kufanya kazi na Awilo na lengo kubwa ni kutangaza utalii wa ndani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz