Amou Haji wa nchini Iran aliyefariki mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 94, anaendelea kushikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtu mchafu zaidi kwa muda wa nusu karne. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, Haji hakuoga kwa takribani miaka 67 na mara kadhaa alishinikizwa kuoga na kupewa maji safi ambapo jaribio hilo lilimhuzunisha sana.
Baada ya majaribio kadhaa kumtaka kufanya hivyo, hatimaye akakubali na baada ya muda mfupi akaugua na kufariki dunia siku ya Jumapili katika kijiji cha Dejgah nchini Iran.
Enzi za uhai wake, Haji alifanya mahojiano na gazeti la Tehran Times mwaka 2014 na kueleza kuwa alikuwa anaishi katika shimo la ardhini na kibanda cha matofali kilichojengwa na wakazi wa kijiji cha Dejgah.
Alipohojiwa kuhusu kuoga, Haji alifuguka kukataa kuoga na kusema kuwa hajatumia maji na sabuni kwa takribani miaka 67, hivyo anahofu huwenda akapata ugonjwa.