Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Avatar kuingizwa Playstation 5

Avatar James Cameron Avatar kuingizwa Playstation 5

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Avatar Frontiers of Pandora inakuja kwenye PlayStation 5 mnamo Desemba 7, ikiwapa mashabiki nafasi ya kucheza kama Na'vi na kupigana dhidi ya Utawala wa Uendelezaji wa Rasilimali RDA (Resource DevelopmentAdministration) ili kulinda mwezi wa Pandora.

Wachezaji wa PlayStation watapokea Kifurushi cha Aranahe Warrior bila malipo, ambacho kinawapa seti za silaha mbalimbali.

Wachezaji watacheza kama Na’vi, ambaye akiwa mtoto mchanga alitekwa nyara na RDA ili awe sehemu ya Mpango wao wa Ambassador Program (TAP) na kupata mafunzo kwanjia za kibinadamu.

Katika trela mpya hii inayoangazia hadithi ya game hili, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu safari ya shujaa huyu ambaye anatafuta kuunganishwa tena na urithi wao uliopotea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live