Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aunty: Sikupanga kumfunika yeyote

Aunty Nandy  . Aunty: Sikupanga kumfunika yeyote

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aunty Ezekiel; ni supastaa wa Bongo Movies ambaye wikiendi iliyopita aling’ara kama staa wa kike aliyependeza kuliko wote kwenye harusi ya mastaa wawili wa muziki Bongo, Nandy na Billnass.

Hata hivyo, Aunty ambaye ni mama wa watoto wawili, anasema kuwa, hakufanya hivyo kwa lengo la kumfunika mtu yeyote.

Akizungumza, Aunty anasema kuwa, alishangaa tu kuona anapongezwa ambapo alichukulia kawaida, lakini kadiri muda ulivyosonga ndipo akaona kama maoni yamekuwa mengi.

“Huwezi kuamini, wakati najiandaa na kuchagua namna nitakavyovaa sikupanga wala sikuwa na wazo la kwamba ninakwenda kumfunika mtu yeyote kwa sababu ni kawaida yangu kuvaa na kupendeza,” anasema Aunty mwenye rangi yake ya chokoleti.

Katika tukio hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mastaa wa kike walijitahidi kuvaa kwa ajili ya kuteka shughuli kuanzia Nandy mwenyewe, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Zmaradi na wengine wengi, lakini Aunty ndiye aliyeibuka nyota wa mchezo.

Wengi waliomuona walikiri kwamba gauni la rangi ya chungwa lilimkaa mno ambapo mastaa wengi wamemsifia kwa kupendeza hadi kumfunika bibi harusi.

Ikumbukwe kwamba, umbo namba nane alilonalo Aunty, awali hakuwa nalo bali amelipapata baada ya kudaiwa kufanya sajari mbili za tumbo na kalio huko nchini India.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live