Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aunty: Sijawahi na sina ugomvi na Ruby

Aunty Ezekiel Er Aunty: Sijawahi na sina ugomvi na Ruby

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aunty Ezekiel; ni kinara wa Bongo Movies na ni baby mama wa msanii wa Bongo Fleva, Kusah ambaye anasema kuwa, hajawahi kuwa na ugomvi na msanii Ruby kama ambavyo inaelezwa.

Ugomvi wa Aunty na Ruby uliibuka mara tu baada ya Aunty kudaiwa kumkwapua Kusah ambaye awali alikuwa akiishi na kuzaa na Ruby mtoto mmoja wa kike aitwaye Aliyah.

Kuhusu sakata hilo, Aunty anasema; “Sijawahi kuwa na ugomvi na yeye kwa sababu uzuri ni kwamba, mimi na yeye hatujawahi kugombea kitu chochote. Hata Kusah sikumkuta kwake, nilimkuta tu chini ya mti, nikamuinua, nikaanza upya.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live