Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aunty Ezekiel amkataa Ruby "Nitaua"

Ruby Sa.png Aunty Ezekiel na Ruby

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja kati ya mahusiano yanayowavutia wengi ni ndoa ya Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara na wake zake wawili kwa namna ambavyo anavyoonesha mitandaoni na watu wengi kuvutiwa nayo.

Kupitia moja ya picha ya watatu hao mtandaoni (Manara na wake zake), imepostiwa pia kwenye ukurasa wa Aunty Ezekiel ambaye huyu ni staa kunako Bongo Movie, na kuipamba picha hiyo kwa ujumbe "Kaka yangu na mawifi zangu".

Ujumbe huo wa Aunty ulimkosha Manara na kukomenti akitoa ushauri kuwa kama vipi mpenzi wa sasa wa Aunty Ezekiel ambaye ni Kusah arudiane na mpenzi wake wa zamani, mwimbaji Ruby ili wawe wawili pia maana watapendeza, kitu ambacho Aunty Ezekiel hajakubalina nacho kabisa, akidai ikitokea hivyo ataua mtu.

"Kusah anapaswa aniige kaka yake, amrudishe Ruby muwe wawili, tena nyie mtapendeza mno..." - ameandika Haji Manara na Aunty Ezekiel kumjibu kwamba, "Naua".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live