Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aunty Ezekiel: Ukitaka kufa mapema, chukua umaskini, changanya na wivu

Aunty Ezekiel Er Aunty Ezekiel

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji mkongwe kutoka Bongo Movies, Aunty Ezekiel amekuja na jipya, kwa kuwapa mashabiki wake mbinu rahisi ya kuishi maisha marefu ama kufa mapema kwa wenye nia ya kufa, lakini kifo kimewakataa.

Aunty ambaye ni mama wa watoto watatu anasema, ukitaka kufa mapema basi ni rahisi kama kuhesabu tarakimu moja mbili tatu, kwani unachanganya umaskini pamoja na wivu kwenye kikombe kimoja kisha unaongezea ushindani, na hapo utakuwa umekikaribisha kifo kwa njia rahisi sana.

“Ukitaka kufa mapema tu changanya umaskini na wivu basi ongeza ushindani, niamini mimi, hata madaktari hawatajua kiini cha kifo chako,” aliandika Aunty Ezekiel.

Mwanamama huyo ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza kwenye filamu mbali mbali na muigizaji marehemu Steven Kanumba alionekana kutupa dongo kwa wanamuonea gere katika mafanikio ya maisha yake.

Katika picha nyingine aliyoiposti katika Ukurasa wake wa Instagram, Aunty amesema; “Tunaishi Dunia ambayo rafiki zetu wanachukia mafanikio yetu kuliko adui zetu,” aliandika Aunty Ezekiel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live