Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aunt Ezekiel: Sijafuata Mkumbo

Aunt Eze.png Aunt Ezekiel

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

AUNT Ezekiel Grayson Jujuman ni staa mkubwa wa Bongo Movies amekiri kwenda nchini India kwa ajili ya kufanya upasuaji wa kurekebisha umbo lake (sajari).

Kwa sasa sajari ndiyo habari ya mjini ambapo Aunt ambaye pia ni mjasiriamali anasema kuwa, hakulazimishwa na mtu yeyote kwenda kufanya hivyo, bali alichagua mwenyewe kwa ajili ya kutengeneza mwili wake na siyo kwamba amefuata mkumbo wa baadhi ya mastaa wenzake.

Aunt ambaye kwa sasa ana kiuno-dondora anasema kuwa, anafurahia alichofanya kwani ni kitu kinachompa furaha ya nafsi siku hadi siku ndiyo maana alitoa pesa kuutengenza mwili wake jinsi anavyopendezwa yeye.

“Unajua watu wengi sana ukienda Uturuki au India wanajua wazi kuwa umeenda kwa ajili ya mtu f’lani, lakini siyo kweli kabisa. “Mimi nilikwenda na sikufuata mkumbo wa mtu yeyeyote yule zaidi ya mimi kutaka kupendeza,” anasema Aunt ambaye ni mama wa watoto wawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live