height="400" Babu Tale, Diamond na Mkubwa Fella katika BET 2016
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa wasanii kutoka Tanzania kutokuwepo katika kipengele cha Best Best International Act baada ya Diamond kuwania kwa mwaka 2014/16.
Soma Pia: Tuzo za BET 2018: Afrika Mashariki hakuna msanii aliyetajwa, Nigeria na SA zaongoza
Sasa basi, June 21, 2017 katika mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond alizungumzia kutochaguliwa kwa mwaka huo na kuhaidi mwaka huu (2018) angekuwepo kutokana na ngoma alizokuwa tayari amezirekodi. (msikiliza hapa chini)
“Mwakani ni lazima niingie, ukiangalia kwanza mwaka jana ulikuwa ni mwaka wa kuwashika vijana wa Kitanzania (WCB) kuhakikisha wanasikika katika muziki na ili wasikike inabidi nipunguze kasi yangu kwa sababu mimi huwa naachiaga tu mawe, kwa hiyo ningeachia ingeleta mtafaruku,” alisema Diamond.
Swali la B Dozen: Wengi wanaogopa isije ikatokea kama ilivyotokea kwa 50 Cent, kabla hajaanza kuwatambulisha G Unit alikuwa anafanya vizuri sana lakini baada ya kuwa G Unit akashuka akawa haonekani kama msanii bali mfanyabiashara huoni kama itakuja kukuathiri kwenye miaka ya baadaye?.
Jibu la Diamond: Nafikiri tu ni kujifunza, uzuri mimi sanaa yangu natumia kujifunza kupitia mifano ya wasanii wa Tanzania na wa nje, ukiangalia kama huu mwaka nimerekodi nyimbo hit karibia 30 za uhakika local na international, so nimejipanga vizuri.
Tangu June 21, 2017 Diamond ameweza kufanya ngoma kadhaa kubwa za kimataifa kama Fire ft Tiwa Savage, Hallelujah ft Morgan Heritage, Waka ft Rick Ross na African Beauty ft Omario. Kwa mara ya kwanza Diamond alichaguliwa kuwania BEA ilikuwa mwaka 2014.