Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa Jela na viboko 74 kwa kukosoa vazi la Hijabu

Mehdi Yarrahi Mwimbaji wa miondoko ya Pop, Mehdi Yarrahi

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya nchini Iran, imemhukumu mwimbaji wa miondoko ya Pop, Mehdi Yarrahi kifungo cha miaka miwili na miezi minane jela na kuchapwa viboko 74, baada ya kuachia wimbo unaokosoa vazi la hijabu ambalo wanawake wanalazimishwa kulivaa nchini humo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa wimbo huo unaoitwa Roosarito unapinga maadili na desturi za jamii ya Kiislamu yenye idadi kubwa ya watu nchini humo.

Yarrahi mwenye umri wa miaka 42, alikamatwa Agosti, mwaka jana kwa tuhuma za kusambaza wimbo huo lakini aliachiwa kwa dhamana Oktoba mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live