Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atumia wimbo wa Davido kupiga Mkwanja

Davido Pics Atumia wimbo wa Davido kupiga Mkwanja

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii Bongo kutikisa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ngoma za wasanii wengine kwa kuzifanyia cover, ndivyo ilivyotokea kwa kijana kutoka nchini Nigeria, Emmanuel Ogbole, maarufu kama Emzy Pondeck.

Emzy amejipatia umaarufu mkubwa unaomfanya apige pesa ndefu kwa kufanya 'show' ya cover ya wimbo uitwao 'Kante' wa mwanamuziki Davido ambao upo kwenye albamu yake ya Timeless.

Kibogo bongo pia wapo wasanii ambao walianza kufuatiliwa baada ya kuanza kufanyia cover nyimbo za wasanii maarufu, kati ya wasanii hao wakiwemo Dayoo, Anjela.

"Kante' ni wimbo wa kumi kati ya nyimbo 16, kwenye albamu ya Davido iitwayo 'Timeless' iliyotoka mwaka 2023, huku nyingine zikiwemo 'Over Dem', 'Godfather', 'Unavailable' na 'Away'. Hadi sasa wimbo huo kwenye YouTube channel ya Davido unawatazamaji milioni 6 ukiwa na miezi tisa tangu utoke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live