Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Atumia ndege kwenda na kurudi chuoni

Mwanafunzi Canada Atumia ndege kwenda na kurudi chuoni

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tim Chen ambaye ni mwanafunzi wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha British Columbia (UBC), kilichopo katika Jiji la Vancouver nchini Canada, ameamua kutumia usafiri wa ndege kwenda Chuoni na kurudi nyumbani kwao Calgary, anapoishi na wazazi wake.

Akizungumza na Kituo cha Runinga cha CTV, Chen amesema, alichukua uamuzi huo kutokana na kupanda kwa kodi ya chumba alichokuwa akiishi katika Jiji hilo, ambayo ilifikia Dola 2,500 sawa na Tsh. 6,369,445/= kwa mwezi, jambo ambalo hakukubaliana nalo na kuamua kutafuta njia mbadala.

Chen ambaye ana vipindi viwili kwa wiki kwenye Chuo hicho, amesema kwa kutumia usafiri wa ndege kwenda Chuoni na kurudi nyumbani, anatumia takribani Dola 150 sawa na Tsh. 382,166/= ambayo kwa mwezi ni Dola 1,200 sawa na Tsh. 3,057,333/=, gharama ambayo amesema ni ndogo zaidi akilinganisha na kodi ya nyumba.

Hata hivyo, Jiji la Vancouver limeeendelea kuongoza kwa kuwa Jiji lenye gharama kubwa zaidi katika nyumba za kupanga nchini Canada.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live