Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Attitude kuvunja rekodi ya Waah?

Attituid Harmo Pic Data Attitude kuvunja rekodi ya Waah?

Sat, 1 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

APRILI 23 mwaka huu msanii wa Bongofleva, Harmonize aliachia wimbo wake mpya ‘Attitude’ ambao ameshirikiana na H. Baba na gwiji kutokea DR Congo, Awilo Longomba. Wimbo huu umekuja wakati bado Diamond Platnumz anafanya vizuri na wimbo ‘Waah!’ aliomshirikisha Koffi Olomide kutoka Congo pia.

Harmonize ambaye alitolewa kimuziki na Diamond kupitia WCB Wasafi na kuondoka hapo, kitendo chake cha kufanya wimbo na Awilo kimetafsiriwa kama uchokozi wa kimuziki kwa bosi wake huyu wa zamani, jambo liloibua ushindani kwa mashabiki wa pande zote mbili.

Hilo linafanya kolabo ya Harmonize na Awilo kutazamwa kwa jicho la tatu kama itaweza kufanya vizuri kama ile ya Diamond na Koffi. Kipimo kinachotumika kuangalia mpambano huo ni namna wimbo husika umepata kutazamwa (views) zaidi kwenye mtandao wa YouTube ambao ndio umekuwa ukitumika na wasanii wengi nchini.

Ukweli ni kwambo wimbo ‘Waah!’ ulifanya vizuri kwa kiasi kikubwa na kujiwekea rekodi zake za kipekee ndani ya Bongofleva kupitia YouTube. Kutokana Harmonize kashajipambanua kama mshindani wa Diamond kimuziki, ana kazi ya kuzivunja rekodi hizo na ikibidi kuweka mpya kupitia kolabo yake na Awilo.

1. Rekodi

aliyovunja

Kolobo ya Harmonize na Awilo ‘Attitude’ ilipoachia tu bila video, iliweza kupata watazamaji 100,000 YouTube ndani ya dakaki 44 pekee na kuweza kuivunjilia mbali rekodi iliyokuwa ikishiliwa na Diamond.

Ikumbukwe Diamond alipotoa wimbo ‘Waah!’ akiwa na Koffi, aliweza kujikusanyia watazamaji 100,000 YouTube ndani ya dakika 48 na kuwa wimbo wa kwanza wa Bongofleva kufanya hivyo. Tofauti hapo ni dakika nne tu.

2. Rekodi

alizoshindwa

Licha ya mafanikio ya awali, Harmonize ameshindwa kuzifikia na kuzivunja rekodi tatu za mwanzo ambazo tayari Diamond alikuwa ameziweka kupitia ‘Waah!’. Nazo ni;

(a). Kufikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa nane.

(a). Kufikisha watazamaji Milioni 4 ndani ya saa 48.

(c). Kufikisha watazamaji Milioni 10 ndani ya siku saba (wiki moja).

3. Rekodi zilizosalia

Kwa sasa Harmonize kupitia video ya wimbo ‘Attitude’ anapambana kuona kama ataweza kufikia na kuzivunja rekodi tano zilizosalia alizoziweka Diamond kupitia wimbo wake, Waah!. Rekodi zilizosalia ni kama ifutavyo;

(a). Kufikisha watazamaji Milioni 20 ndani ya wiki tatu.

(b. Kufikisha watazamaji Milioni 30 ndani ya mwezi mmoja.

(c). Kufikisha watazamaji Milioni 40 ndani ya miezi miwili.

(d). Kufikisha watazamaji Milioni 50 ndani ya miezi mitatu.

(e) Kufikisha watazamaji Milioni 60 ndani ya miezi minne.

Endapo Harminize atafanikiwa kufikia au kuvunja rekodi hizo, bado anakabiliwa na mtego mmoja kutoka kwa Diamond, nao ni kuweka hadharani kiasi cha mauzo alichopata YouTube kutoka kwenye wimbo huo (Attitude) kama alivyofanya Mondi kwenye wimbo, Waah!. Hivi karibuni Diamond alisema video ya ‘Waah!’ ilipofikisha watazamaji Milioni 39.3 ikiwa ni takribani miezi miwili tangu itoke, iliweza kumuingizia Euro 32,266 sawa na Sh 89.8 Milioni.

Imeandikwa na Peter Akaro

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz