Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Atiwa hatiani kwa kutangaza kuuza fimbo ya Malkia Elizabeth II

Malkia Elizabeth Fimbo Atiwa hatiani kwa kutangaza kuuza fimbo ya Malkia Elizabeth

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Southampton nchini Uingereza imemkuta na hatia ya ulaghai, Dru Marshall mwenye umri miaka 26, mkazi wa Hampshire kusini mwa Uingereza, baada ya kijana huyo kutangaza kupitia ebay, kuuza kile alichodai kuwa ni fimbo (mkongojo) iliyokuwa ikitumiwa na Malkia Elizabeth II.

Imeelezwa kuwa Kijana alitengeneza mnada wa kuuza fimbo hiyo, kupitia ebay na kusema kuwa yeye ni moja ya wafanyakazi katika Kasri la Windsor, na mapato yatakayopatikana baada ya kuuza fimbo hiyo yangeenda kwenye utafiti wa magonjwa ya saratani na kwamba tayari mnada huo ulikuwa umefikia pauni 540 sawa na Tsh. 1,728,338/=, kabla hajausitisha baada ya kugundua kuwa anafuatiliwa na Polisi.

Malkia Elizabeth II, aliyehudumu muda mrefu zaidi nchini Uingereza, alifariki Dunia Septemba 8, 2022 akiwa Balmoral akiwa na umri wa miaka 96, baada ya kutawala kwa miaka 70.

Malkia alishika kiti cha ufalme mnamo 1952 na alishuhudia mabadiliko makubwa ya kijamii.

Kutokana na kifo chake, mwanawe wa kwanza Charles, mwanamfalme wa zamani Wales alishika hatamu ya kuongoza nchi kama Mfalme mpya na mkuu wa nchi kwa milki 14 za Jumuiya ya Madola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live