Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Athari unayoweza kupata ukianza kuzaa baada ya miaka 35

Lactancia 1 E1635184742640 Athari unayoweza kupata ukianza kuzaa baada ya miaka 35

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanaume wanaoamua kuwa wazazi baada ya miaka 35 wanakabiliwa na uwezekano wa hatari ya kupata watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa au wenye hali ya usonji (autism).

Pia kila mwaka unaokwenda, mbegu za uzazi za kiume hupungua kwa kiasi kikubwa kwa wingi na ubora wake, jambo linaloweza kuhatarisha uwezo wao wa kuendeleza kizazi.

Haya yamebainishwa na tafiti kadhaa zilizofanywa katika miaka ya hivi karibuni, ukiwemo utafiti uliofanywa na kitivo cha tiba cha Chuo kikuu cha Stanford University, nchini Marekiani, ambacho kilitathmini data kutoka kwa uzazi zaidi ya milioni 40.

Kuhusu uzazi na taarifa (chache zinazofahamika ) kuhusiana na taarifa hii , habari njema ni kwamba kuna mapendekezo, vipimo na tiba ambayo inaweza kufuatilia kwa karibu na kupunguza hatari kwa mtoto wako mchanga.

Daktari Karla Giusti Zacharias, mtaalamu aliyebobea katika masuala ya uzazi wa binadamu na mjumbe timu ya tiba katika Rede D'Or - São Luiz Itaim Hospital katika São Paulo, anaelezea kwamba mara kwa mara hupokea wanaume katika ofisi yake ambao wangependa kuwa na watoto . .

"Ninawapokea wagonjwa wenye miaka 50 na ushee na 60 na ushee ambao wanawaoa wanawake vijana ambao wanataka kupata ujauzito ," anasema. Swali wanalouliza kwa wanaowatibu ni kwamba : ni zipi hatari za baba mwenye umri mkubwa ? Kwa ujumla, mfumo wa uzazi wa mwanaume hutenda tofauti kabisa na ule wa wanawake.

Huku wanawake wakiwa na ukomo wa idadi ya seli za uzazi, kwa wanaume utengenezwaji wa mbegu za uzazi- ambao huanza katika kipindi cha kubalehe - huendelea katika kipindi chote cha maisha yao.

Na hapa ndipo jambo muhimu hujitokeza: ingawa uzalishaji wa mbegu za uzazi haukomi, ubora wa mchakato huu hauwi sawa baada ya umri fulani.

Kadri miaka inavyokwenda, na jambo halisi kwamba seli hizi hutengenezwa kwa kiwango kidogo zaidi na huwa na kasoro zaidi.

Kasoro hizi , matokeo yake zinaweza kuzuia utungwaji wa mimba . Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa hata wakati wanapofanikiwa kuwa na uwezo wa kutungisha mimba, mtoto mchanga anakuwa katika hatari ya kupata matatizo ya mara kwa mara ya kiafya kuanzia kasoro katika mfumo wa kupumua hadi autism.

Utafiri uliofanywa katika mwaka 2018 na Chuo kikuu cha Stanford cha tiba ulibaini kwamba kwa ujumla, kadri mwanaume anavyoendelea kuwa na umri mkubwa, ndivyo ndivyo mtoto anavyokuwa na uwezekano wa harari ya kuzaliwa akiwa na kasoro za kiafya.

Wanaume wenye watoto baada ya umri wa miaka 35, wana uwezekano wa juu zaidi wa watoto wao kuzaliwa wakiwa na uzito wa chini wa mwili, kuwa na kifafa, au kuhitaji kuongezewa hewa ya kupumua muda mfupi baada ya kuzaliwa.

 Watu wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wana uwezekano wa 14% zaidi wa kupata watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda wao kufika o, na wale wenye zaidi ya umri wa miaka 50 wana uwezekano wa 28% zaidi watoto wao wanaozaliwa kuhitaji kuwekwa katika kitengo cha matibabu ya dharura (Intensive care unit) kwa muda.

Katika chapisho hilo hilo Michael Eisenberg, profesa wa masuala ya uzazi na mkuu wa utafiti, anabainisha kwamba idadi hiyo haipaswi kufasiliwa kama kitu cha kutisha. Anasema , matokeo ya utafiti huu yanapqasw akusaidia familia kupanga vyema na kufuatilia afya yao ya uzazi kadri inavyopaswa.

  Katika hitimisho, utafiti huo unabainisha kuwa, kwa kila miaka 10 ya ongezeko la umri wa baba, kuna 21% ya fursa ya ziada kwamba mtoto ataugua kutokana na hitilafu, zinazohusiana na ugumu wa kuwasiliana, maingiliano ya kijamii na kitabia.

Sayansi bado haijajua ni kwanini hili linatokea.

 Lakini licha ya kupungua kwa ubora wa mbegu za uzazi za kiume na idadi yake suala ni uimara wa mfumo wa seli za uzazi na moja wapo ni kuweza kutungisha mimba, kupunguza hatari za kiafya. za mtoto, anaeleza Alfredo Canalini, rais wa chama cha madaktari wa uzazi cha Brazil.

 Mr. Canalini anasisitiza kuwa hakuna uwezekano wa kuepuka athari za kuchelewa kuwa baba.

“Baiolo ya mfumo wa uzazi wa kike unategemea na mtu binafsi wa kiwango cha juu na mwanaume anahitaji ushauri wa daktari kuelewa ni nini kinachoendelea na ni kipi kinapaswa kufanyika ,” anasema.

Wanaume wanaotaka kuwa mababa wazee wanapaswa kupima uzito wa kumkuza mtoto. Ushauri huo unahusisha daktari wa kawaida au daktari wa uzazi.

Tathmini hiii inaweza kufanywa mara moja, kila mwaka, wakati panapokuwa na dalili fulani, kama vile kukasirika kusiko kwa kawaida, ugumu katika kupata ari ya kujamiiana au kupatwa na ari hiyo kwa kipindi kifupi pamoja na kushindwa kutungisha mimba.

Zacharia tunapoona mabadiliko fula katika mtindo wetu wa maisha antukumbusha, inawezekana kuanza vipimo fulani na matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live