Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Asoma Taarifa ya Habari kwenye TV na mtoto mgongoni

Mtangazaji Mgongoni Kapinga Kisamba Clarisse

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa kike wa Televisheni mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kapinga Kisamba Clarisse amejizolea umaarufu baada ya kuonekana akiwa anasoma taarifa ya habari akiwa amembeba mtoto wake mgongoni.

Tukio hilo lilitokea katika kituo cha Televisheni kilichopo Goma, Mashariki mwa DR Congo.

Kwenye mitandao ya kijamii, Clarisse amepongezwa kwa kitendo hicho wakisisitiza umuhimu wa kuwasaidia kina mama wanaofanya kazi katika mazingira magumu.

Tukio hilo lilitokea Machi 8, 2024 wakati dunia ilipoadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live