Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aslay kulipua goma jipya leo

Aslay Kulipua Goma Jipya Leo Aslay kulipua goma jipya leo

Fri, 27 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ‘Follow Me’ aliyoshirikiana na Harmonize na ‘Mouzzah’ kutoka miezi miwili iliyopita, nguli wa muziki nchini Tanzania Aslay anatarajia kuachia kazi yake mpya iitwayo ‘Inauma’, ifikapo tarehe 27 Januari, 2023.

‘Inauma’ ni wimbo wa mapenzi lakini wenye kusikitisha na kuumiza moyo, wimbo huu una mahadhi ya mpangilio wa ara za muziki wa zamani wa kitanzania utakaoweza kukupa hisia kali sana. Katika wimbo huu, Aslay amezungumzia wivu, ambapo unapelekea kushindwa kuvumilia pale unapoachwa na Yule umpendaye kwa dhati.

Kama ujuavyo Aslay ni mwandishi bora kabisa anafanya kazi kubwa ya kupangilia maneno katika tungo zake,katika uandishi huu unaongeza utofauti kwenye wimbo, na kuweka ucheshi uliotumika unafanya wimbo kuwa wakipekee vinginevyo ungekuwa wimbo wa mapenzi wa kusikitisha, lakini ucheshi umenogesha na kuufanya wimbo wa kufurahisha na kuumiza katika mapenzi.

Aslay kwa sasa yupo chini ya lebo kubwa ya muziki Afrika ijulikanayo kama Sony Music Africa na kazi zake zikisimamiwa na Rock Star Africa. Hakika mwaka 2023 ni mwaka mwingine wa kijana huyo kukonga mioyo ya mashabiki zake na wapenzi wa muziki wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live