Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aslay arejea upya kwa kishindo

Aslay Ub Aslay arejea upya kwa kishindo

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ukimya wa muda mrefu, hatimaye yule msanii mkongwe aliependwa na anaezidi kupendwa na kila mja Aslay amefunguka na kusema kuwa mashabiki zake wategemee makubwa sana kutoka kwake.

Aslay ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa; “Ninafuraha kuwaambia Mashabiki, Vyombo vya habari na kila anayenifuatilia kwamba hivi karibuni nimejiunga na RockStar Africa. Imekuwa safari ndefu yenye matumaini makubwa katika kusimamia kazi zangu za muziki,” ameendelea kwa kuandika kuwa;

“Hivyo basi, Nawaarifu kutegemea mengi makubwa katika muziki wangu na kuniona katika hatua kubwa zaidi. Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipindi chote ambacho nilikuwa kimya, hakika nimejifunza Mengi.

“Ningependa kuchukua wakati huu Pia kutoa shukrani zangu kwa kila mmoja wenu kwa support mnayoendelea kunipa katika muziki wangu hata wakati nilipokuwa kimya niseme tu Asanteni sana,” ameandika Aslay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live