Siku chache baada ya staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kusema kama akipewa Aslay amsimamie angekuwa mbali, msanii huyo ameibuka na kuonesha kwamba siyo kinyonge, yupo vizuri.
Kupitia ukurasa wake, Aslay ambaye alikuwa kimya kidogo kwenye gemu, ameposti bonge la studio na kuandika maneno machache kuinadi studio hiyo.
“Ukubwa wa Mungu haufanani na kitu chochote ndugu zangu. Na hii ndio ofisi yangu ni studio yangu kabisaaa mnakaribishwa mfungue makoo yenu,” alimaliza Aslay na kuweka emoji ya kushukuru.
Diamond alitoa kauli hiyo kwenye uzinduzi wa albamu ya Barnaba ya Love Sound Different katika ukumbi wa Mlimani City alipokuwa akieleza ni jinsi gani muziki unahitaji uwekezaji wa fedha kwani wapo wasanii wakubwa na wenye uwezo lakini hawapati mafanikio makubwa sababu hakuna watu waliowekeza fedha kwao.