Watu wengi wanaelewa damu ni nzito kuliko maji ila kwa Jane Wanjiku, dada zake ndio waliomharibia maisha.
Wanjiku alisema aliolewa na dereva wa baba yake, asijue atamharibia maisha.
"Niliolewa baada ya kuhitimu kidato cha nne. Aliyenioa alikuwa ni dereva wa baba'ngu. Nilikwenda kuishi naye Eldoret na nikakuta nguo za mtoto nyumbani kwake, lakini aliniambia kwamba ni za dadake.
"Nilipoulizia niliambia kwamba ana mke ambaye aliondoka wiki moja kabla ya ujio wangu. Mkewe aliporudi tulikorofishana na kuamua kuondoka. Alimuacha na mwanaye wa miezi sita na hatimaye mume wangu alimpeleka kwa wazazi wake," Wanjiku alisimulia.
Wanjiku alisema kwamba ingawa alijaribu kumsaidia mumewe alipokuwa hana chochote, baadaye alimuona kama takataka.
Kulingana na mwanamke huyo, mumewe alikuwa na uhusiano na wanawake wengi na watoto 12, na hatimaye alimtema na kuamu kuishi na dadake.
"Nilipata kazi Nairobi na kurejea mtaani Umoja. Nilimuambia nataka niwe peke yangu. Aliketi na dada zangu na sijui walichoongea. Alianza kusihi na mmoja wa dada zangu. Alibeba vyombo vyote vilivyokuwa nyumbani kwangu na kuanza kuishi na dada'ngu ambaye ana mume," Wanjiku alisema.
Mwanamke huyo aliyevunjika moyo alimuambia Kagoni kwamba aliyekuwa mumewe, alikuwa na haja na mali yake, na dada zake walimtumia mumewe aliyempenda kuharibu maisha yake.