Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashura Maulid mwandishi wa habari anayemwakilisha Sinyora Gabriella

Fri, 11 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ashura Maulid

Ashura ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, katika tamthilia hii mbali na kunakilisha Sinyora Gabriela, pia anawanakilisha Efsun na Daktari Hellena.

Wakati Daktari Hellena yeye akiwa ni Daktari wa familia ya Sultani, Efsun Hatun aliingia kwenye kasri kama kijakazi wa Hurrem Sulan akiwa anajulikana kwa jina la Nora.

Lakini baadaye aliingia kwenye mahusiano na Shehazard Mustafa na baadaye akajikuta anapata mimba, lakini mama wa Mustafa Mahdevran Sultana hakuyabariki mahusiano hayo na kufanya juu chini kumtoa mimba ambapo binti huyo alipoteza maisha.

Ashura anasema akiwa kama mtangazaji anasikia amani kutumia sauti yake katika upande mwingine wa kunakilisha sauti.

“Napenda kutumia sauti yangu kwa kuwa najua nina uwezo wa kuichezea vile ninavyotaka, ”anasema.

Moja ya mambo ambayo hayapendi katika tamthilia hiyo ni ubabe.

Anawaasa watu kutoishi maisha kama yaliyomo ndani ya tamthilia hiyo kwa sababu hayapendezi.

Wakati analovutiwa nalo ni namna wamama wanavyowapenda watoto wao na wanavyoumia pale ambavyo wanapotendewa ndivyo sivyo akiwemo Hurrem na Mahdervan.



Chanzo: mwananchi.co.tz