Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arnold Schwarzenegger kurudi kwenye Televisheni

Arnold Schwarzenegger.jpeg Muigizaji mkongwe wa Marekani Arnold Schwarzenegger

Fri, 29 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji mkongwe wa Marekani Arnold Schwarzenegger (76), amesema yuko tayari kurudi kwenye televisheni mwezi ujao baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo wiki iliyopita.

Katika upasuaji huo Gavana huyo wa zamani wa California amewekewa kifaa (pacemaker) kitakachosaidia moyo wake kufanya kazi sawasawa.

Japokuwa hatoweza kufanya mazoezi mazito kwa muda mrefu Muigizaji huyo amesema yuko fiti na ataendelea kurekodi msimu wa pili wa “Fubar”, inayoonekana kupitia Netflix.

Schwarzenegger alizaliwa na tatizo la moyo na amewahi kufanyiwa upasuaji mwingine mwaka 1997, 2018 na 2020.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live