Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arnelisa wa Ben Pol: Sijashiriki mapenzi mwa miezi saba

Anerlisa Muigai Photossss Anerlisa Muigai

Tue, 28 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binti wa Seneta wa Nakuru Tabitha Karanja, Anerlisa Muigai sasa anadai kuwa hajashiriki tendo la ndoa (mapenzi) kwa miezi saba sasa.

Machi 23, mwaka 2023 Anerlisa alipuuzilia mbali madai kuwa ameathirika kivyovyote na hali hiyo.

"Nimepiga miezi saba bila kushiriki kwichi kwichi na bado niko vizuri tu. Kwanza niko bora na mtazamo wangu kuhusu kila kitu umebadilika," Anerlisa alisema.

Anerlisa aliingia katika mahusiano na mwanamuziki wa Tanzania, Ben Pol mwaka 2018 na wawili hao kufunga pingu za maisha mnamo Mei 2020.

Tufuatilie kwenye Instagram pata habari muhimu zaidi moja kwa moja kwenye app yako uipendayo! Hata hivyo ndoa yao ilikumbwa na misukosuko chungu nzima, wakiachana Februari 2021 na mengi kusema kuhusu ndoa yao ambayo haikudumu.

Anerlisa atangaza mpenzi wake mpya Baada ya kutemana na Ben Pol Februari 2021, Anerlisa hakuchukua muda mrefu kabla ya kuzama katika penzi jingine.

Alimtambulisha mpenzi wake mpya kwa jina Melvin Ibrahim na kumtangaza waziwazi kama mwanamume aliyeuteka moyo wake. Katika mahojiano na Word, Anerlisa alisema kuwa awali alidhani kuwa kila mwanamume aliyetoka naye kimapenzi alikuwa na nia ya kweli.

"Hilo lilifanya nisione taswira kamili," Arnelisa amenukuliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live