Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apata upofu baada ya kuchora tattoo kwenye mboni za macho yake

Anaya Peterson Anaya Peterson

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo mmoja mwenye umri wa miaka 32 aliyetambulika kwa jina la Anaya Peterson amepoteza uwezo wake wa kuona baada ya kuchora tattoo kwenye mboni za macho yake (eyeballs).

Anaya alishawishika kuchora tattoo hizo kutoka kwa mwanamitindo Amber Luke. Anaya ambaye ni raia wa Ireland Kaskazini amepata upofu wa moja kwa moja kutokana na kemikali zilizotumika kuchora tattoo hizo zenye rangi ya Bluu na Zambarau.

Mwaka 2020 Anaya alifanyiwa tattoo katika jicho lake la kulia ili liwe na rangi ya bluu kisha Desemba mwaka huo huo alifanya tattoo nyingine jicho lake la kushoto liwe la rangi ya zambarau.

Mambo yalienda vizuri lakini baada ya muda mambo yakaenda arijojo akaanza kuvimba usoni na maumivu kisha kuanza kupoteza uwezo wa kuona na kuna tishio akawa kipofu kabisa kwa mujibu wa madaktari na kuweza kupata athari nyingine

Amekaa kwa miezi kadhaa bila kuona madhara yoyote lakini mwaka 2021 aliamka na kukuta macho yake yakiwa yamevimba. Mpaka sasa amepoteza kabisa uwezo wake wa kuona.

Hata hivyo inadaiwa kuwa binti yake wa miaka 7 alimkanya mama yake mapema ingawa hakumsikiliza hadi tatizo hilo linampata.

Anaya ameupasua pia ulimi wake kama sehemu ya kutaka kuzidi kuwa mrembo na kuvutia pia kujichora tattoo hadi usoni na kukitoboa baadhibya sehemu za mwili

Anaya ambaye ni mama wa watoto 5, amesema mwanae wa miaka 7 awali alimuonya kuhusu tattoo za macho kuwa sio kitu kizuri na sasa anajuta bora angesikiliza ushauri huo

Kabla, ya kibao kumgeukia, Anaya alipata inspiration ya kufanya tattoo za macho toka kwa mwanamitindo Amber Luke toka Australia anayejulika zaidi kama "blue-eyed dragon" ambaye 2019 alifanyiwa tattoo za kuyafanya machonyake yawe ya blue kisha kupoteza uwezo wa kuona kwa wiki mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live