Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anne Heche afariki dunia, viungo vyake vitatolewa na kusaidia wengine kuishi

FB IM Anne Heche Amne Heche

Mon, 15 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anne Heche; ni staa mkubwa wa filamu wa Hollywood, Marekani ambaye amefariki dunia (kisheria), lakini atabaki kwa muda mfupi kwenye mashine ya kumsaidia kuishi ili timu ya wataalam iweze kuangalia kama kuna viungo vyake vinavyofaa kutumika kwa watu wengine.

Kwa mujibu wa muwakilishi wake, Anne (53) ambaye alipata ajali mbaya ya gari wiki iliyopita alishapanga siku nyingi kuwa akifa angependa kujitolea viungo vyake vinavyofaa viondolewe na kupandikizwa kwa watu wenye uhitaji.

Vipimo vya awali vya damu yake vimeonesha kuwa staa huyo alikuwa ametumia dawa kadhaa ikiwemo cocaine wakati akiendesha gari.

Amewahi kuigiza kwenye filamu kubwa duniani kama Volcano, Psycho, Donnie Brasco na nyinginezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live