Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anjellah avujisha siri: Ibraah anataka kusepa Konde Ganga, maisha magumu

Ubraah 0005 Anjellah avujisha siri: Ibraah anataka kusepa Konde Ganga, maisha magumu

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia moja ya sauti ambayo imevuja na kusambaa mitandaoni huku ikimuhusisha msanii Anjellah ambaye alikuwa KONDE GANG, akitoa siri za lebo hiyo pamoja na maisha yake aliyokuwa anaishi, inadaiwa kuwa Ibraah naye anataka kumkimbia Harmonize.

Kupitia hiyo sauti hiyo, Anjellah amesikika akisema kuwa; "Ibrah nae anataka kuondoka KONDE GANG kwa sababu pale hakuna cha familia kwa sababu maisha ni magumu. Yani pale umasikini unauona kabisa, unaishi pale hupati ata Tsh 100, na ikitokea machawa wamefanya kazi na yeye halafu akapata kimeo kingine Harmonize ananuna.

"Heti kwa nini unafanya hicho kimeo, kumbe ila nia yake anataka ubaki naye halafu akupe Tsh 20,000 wala hajuwi kama una familia," amesema Anjellah.

Anjela amesema kuwa Ibraah akitokea kupata bosi mwingine atatoka Konde Gang kwa sababu Harmonize hawapi wasanii wake pesa zozote.

Ameongeza kuwa Harmonize ana pesa, ila yupo radhi awape wadada pesa zake badala ya kuwasaidia wasanii wa Brand yake ya Konde Gang. Moja ya changamoto alizofichua Anjela ni kuwamba unaweza fanya muziki kwa label hiyo na Harmonize asikupe hata Mia.

Sababu kuu ya Anjela kutoka Konde Gang, kulingana na alichokisema ilikuwa kutumika vibaya kwa kukosa kulipwa huku Harmonize akionga wanawake Range Rover wakati wasanii wake wakiteseka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live