Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anjella aweka rekodi hii mpya

Anjella 1 Anjella aweka rekodi hii mpya

Wed, 16 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Mwimbaji na mwandishi wa nyimbo kutoka lebo ya muziki Konde Music Worldwide (KMW) , Anjella amejikusanyia views zaidi ya Milioni 7.97 kwenye mtandao wa YouTube kupitia maudhui (nyimbo) zake zote.

Submitted by Telesphory on Jumatano , 16th Jun , 2021 Picha ya Msanii Anjella

Mwimbaji huyo alijiunga na mtandao wa YouTube mwezi Oktoba 25, 2020 na amekuwa na wastani wa kutengeneza views zaidi ya milioni 1 kila mwezi kupitia kazi zake mbalimbali ambazo amezipakia kwa takribani kipindi cha miezi 7 na nusu hivi.

Ikumbukwe nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya wiki iliyopita alikabidhiwa Plaque (Silver Button Award) na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha wafuatiliaji (Subscribers) zaidi ya  100,000

Chanzo: eatv.tv