Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anjella alikuwa kipenzi cha Harmonize ila ndio basi tena!

Anjella Mks Anjella alikuwa kipenzi cha Harmonize ila ndio basi tena!

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye aliyekuwa ‘First Lady, wa Konde Music Worldwide yake Harmonize, Anjella ameaga rasmi na kuondoka katika Lebo hiyo baada ya kufanya nayo kazi kwa muda wa mwaka mmoja na miezi 8.

Utakumbuka Anjella alitambulishwa Konde Music Machi 2021 na kuwa msanii wa sita wa lebo hiyo baada ya Ibraah, Cheed, Killy, Young Skales toka Nigeria na Country Boy aliyemaliza mkataba wake.

Hata hivyo, kabla ya utambulisho huo tayari Harmonize alikuwa amemshirikisha Anjella kwenye wimbo wake, All Night ambao ulitoka Februari 16, 2021 na kupata mapokezi mazuri.

Kwa kipindi cha takrabani mwaka mmoja wameweza kushirikiana kwenye nyimbo tano, tangu Harmonize atoke kimuziki Agosti 2015, Anjella ndiye msanii aliyefanya naye kolabo nyingi zaidi tena kwa kipindi kifupi.

Baada ya All Night, Anjella alimshirikisha Harmonize kwenye wimbo wake, Kama ulioachiwa Aprili 11, 2021, kisha Harmonize akamshirikisha tena Anjella kwenye ngoma yake, What Do You Miss inayopatikana kwenye albamu yake ya pili, High School iliyotoka Novemba 5, 2021 ikiwa na nyimbo 20.

Kufika Desemba 18, 2021 Angella akampa shavu Harmonize katika ngoma yake, Toroka yenye mahadhi ya Amapiano, na sasa ameachia wimbo mwingine mpya wa kushirikiana uitwao Kioo.

Lakini katika wimbo mpya wa Marioo, Naogopa aliomshirikisha Harmonize, kuna sauti ya Anjella kwenye vesi ya Harmonize mwishoni, hivyo tunaweza kusema wameshirikiana kwenye ngoma sita.

Ikumbukwe Julai 2021 Anjella alifanikiwa kupata tuzo kutoka YouTube (Silver Button Award) baada ya chaneli yake kufikisha wafutiliaji (subscribers) 100,000 ikiwa ni miezi mitatu tangu atangazwe rasmi kuwa chini ya Konde Music.

Mafanikio hayo yaliifanya Konde Music kumpatia zawadi ya gari aina ya Toyota Crown baada ya kufanya hivyo kwa wasanii wake, Ibraah na Country Boy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live