Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anjella akiri kutoka na Dulla Makabila

DULLA NA ANJELLA Anjella akiri kutoka na Dulla Makabila

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Anjella amesema kuwa yeye pamoja na msanii wa singeli Dulla Makabila walikuwa wapenzi kwa miaka miwili japo penzi lao lilikuwa la siri.

Kwenye mahojiano leo hii Anjella amesema; “Mimi na Dulla Makabila tulikuwa wapenzi kisirisiri kwa miaka miwili japo baadae mwenzangu alikuja kuyaweka wazi. Sababu ya sisi kutengana ni yeye alikuwa na mambo mengi na Ubusy sana maana mimi napenda Time na attention.

“Mahusiano yetu yalikuwa kabla hajaoa lakini alipooa tukabaki mashkaji tu ila alipoachana na Mkewe tukarudiana, japo Mapenzi yetu yalikuwa ‘ya kisela’ sana atazunguka kote lakini anarudi kwangu,” amesema Anjella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live