Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anjela aeleza manyanyaso aliyopitia

44b39ee8a321fb856bfe756fffbd00d4.jpeg Anjela aeleza manyanyaso aliyopitia

Thu, 18 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MSANII chipukizi anayefahamika kwa jina la Anjela kutoka lebo ya Konde Gang amesema katika safari yake ya muziki hatosahau namna alivyokuwa akinyanyasika kutokana na ulemavu alionao.

Nyota huyo anayevuma na kibao chake cha Kama alichomshirikisha bosi wake, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ alisema Dar es Salaam jana kuwa alikuwa akitengwa na baadhi ya watu walioonesha nia ya kumsaidia awali, lakini ndoto zilikuwa hazitimii kwasababu ya hali aliyonayo.

“Nilipitia manyanyaso, kutengwa kwasababu ya miguu yangu wananiambia watachukuaje video kwa matatizo niliyonayo,”alisema.

Anjela aliweka wazi alianza kuugua miguu tangu mwaka 2013 ilikuwa inavimba na alipoenda hospitali tofauti alikuwa akielezwa majibu tofauti kuwa ana matende, wengine ni ugonjwa wa ngozi na kwingine akielezwa kuwa ni mirija ya damu imevimba.

Alisema ilifikia mahali alitaka kukata tamaa ya muziki kwani wazazi wake walimwambia aache kutokana na matatizo aliyonayo yaliyomfanya atengwe na kushindwa kutimiza ndoto zake.

Nyota huyo alisema hakukata tamaa katika muziki aliendelea mbele na anashukuru kwamba Harmonize alitambua kipaji chake na kumchukua kumsaidia kutimiza ndoto zake.

Msanii huyo kwa sasa ameanza kutibiwa miguu na hiyo ni kwa mujibu wa bosi wake Harmonize.

Chanzo: www.habarileo.co.tz