Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angelina Jolie: Niliwahi kuajiri mtu aje kuniua

Angelina Jolie Angelina Jolie

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa filamu wa nchini Marekani Angelina Jolie ni miongoni mwa watu maarufu waliopitia changamoto ya msongo wa mawazo na afya ya akili katika umri wake wa ujana.

Katika mahojiano yake na Jarida la The Face mwaka 2022, amewahi kukiri kuwa alijaribu kujiua katika vipindi viwili tofauti, akiwa na umri wa miaka 19 na akiwa na umri wa miaka 22 ambapo mara hii alimtafuta mtu atakayemtoa uhai ili familia yake isijue kama ni yeye ndio alitaka kujiua.

Jaribio hilo lilishindikana baada ya mtu aliyemtafuta amtoe uhai kuwa na mtazamo tofauti, alimwambia huo sio uamuzi sahihi hivyo afikirie tena upya kisha atampigia baada ya miezi miwili. Hapo ndipo Jolie alibadili mawazo yake na kuruhusu maisha yaendelee hadi leo.

Leo June 4, Angelina Jolie anatimiza umri wa miaka 49 akiwa na watoto 6, kati yao 3 amezaa mwenyewe na 3 wengine ni kwa njia mbadala. Happy birthday Angelina Jolie.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live