Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angel Kato wa BSS mikononi mwa Awilo

Kato Pic Data Angel Kato wa BSS mikononi mwa Awilo

Mon, 10 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mshindi namba nne wa mashindano ya Bongo Star Search (BSS) mwaka 2015, Angel Mary Kato, atua mikononi mwa mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemkrasia Congo, Awilo Longomba.

Awilo ambaye yupo kwa takribani mwezi sasa nchini kwa shughuli za filamu, mbali ya kuigiza na Angel pia wametengeneza naye wimbo.

Leo Jumatatu Mei 10,2021 wawili hao wametangaza ujio wa wimbo wao wa 'Tanzania'  kwa waandishi unatarajiwa kuachiwa leo baadaye.

Akielezea hilo Angel amesema uongozi wake wa lebo ya CShirima ndio umewezesha kufanyika kwa hayo yote kwani kwa uchanga wake kwenye muziki ingekuwa ngumu kumfikia mwanamuziki huyo mkubwa barani Afrika.

Katika wimbo huo Angel amesema wameimba kuhusu maliasili zinazopatikana hapa nchini zikiwemo mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro na madini ya Tanzanite.

"Kupitia nyimbo hii naamini tutaitangaza Tanzania duniani  hususani katika masuala ya utalii kwani Awilo ni msanii mkubwa ndani na nje ya Congo," amesema Angel.

Kwa upande wake Awilo amesema alikubali ombi la Angel kama moja ya zawadi kwa watanzania katika kuitangaza nchi hiyo.

"Tanzania nina historia nayo ni nchi ambayo ninaipenda sana, hivyo kupitia wimbo huu ni zawadi yangu kwao nina amini wataifurahia," amesema Awilo.

Wimbo huo wa Tanzania wamepigia picha za video zake katika milima ya Pugu wilayani Kisarawe, mkoani Pwani

Aidha mwanamuziki huyo amesema mbali na Angel kuimba naye, pia katika filamu ya "No Regret" ambayo ipo mbioni kukamilika amecheza naye kama mke wake.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz