Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anerlisa wa Ben Pol adaiwa kufirisika

Anerlisa BENPOL Anerlisa na Ben Pol

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anerlisa Muigai; ni mrembo maarufu na tajiri nchini Kenya na mke wa zamani (ex) wa staa wa RnB nchini Tanzania ambaye amekuwa gumzo mitandaoni baada ya madalali kuwasili nyumbani kwake, Lavingtone nchini humo kupiga mnada nyumba yake.

Madalali hao wanadai mrembo huyo anadaiwa mali na deni la shilingi milioni 3.3 za Kenya ambayo ni amri ya Mahakama Kuu.

Jana, kupitia mtandao wake wa kijamii, Anerlisa hatimaye alizungumza akisema hakuna mali yake iliyochukuliwa wakati wa uvamizi huo ambao haukufanikiwa.

“Hakuna dalali aliyechukua chochote changu na kuhama kwangu hakuhusiani na mtu yeyote ila mimi mwenyewe. Nilihitaji tu kuweka wazi hilo,” alisema Anerlisa.

Taarifa yake pia ilieleza kuwa hakuhama kwa sababu madalali hao, bali ni kwa sababu shughuli zake nyingi za biashara zinafanyika huko Naivasha na Nakuru ambapo ndiko nyumbani kwa familia yake.

Anerlisa alitangaza kuhama kutoka kwenye nyumba yake huko Lavington na kusema; Siwezi kuamini kwamba ni lazima niondoke nyumbani kwangu Nairobi. Hakika nitakumisi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live